Singida. Watu 29 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa leo baada ya mabasi mawili kugongana huko Maweni wilayani Manyoni Mkoa Singida.
Mabasi hayo yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy, moja lilikuwa linasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lilikuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam.
Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema idadi ya majeruhi bado haijajulikana japo kuwa amesema ni wengi.
"Nikweli ajali imetokea Maweni na tupo eneo la tukio tunaendelea na utaratibu wa kuondoa majeruhi na maiti," amesema Kamanda