Jumatatu, 4 Julai 2016

Ajali iliyohusisha magari 2 ya City Boy yamegongana nakuua

Singida. Watu 29 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa leo baada ya mabasi mawili kugongana huko Maweni wilayani Manyoni Mkoa Singida.



Mabasi hayo yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy, moja lilikuwa linasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lilikuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam.
Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema idadi ya majeruhi bado haijajulikana japo kuwa amesema ni wengi.
"Nikweli ajali imetokea Maweni na tupo eneo la tukio tunaendelea na utaratibu wa kuondoa majeruhi na maiti," amesema Kamanda


Jumapili, 12 Juni 2016

Rais afanya mabadiliko Baraza la mawazili

Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri huku akimteua Mbunge wa Buchosha Dk. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Mawaziri walioteuliwa katika mabadiliko hayo wataapishwa Jumatatu  asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.


Ijumaa, 20 Mei 2016

#HABARI Rais atengua uteuzi wa wazili wa mambo ya ndani

Rais‬wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo yaNdani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Jumatano, 18 Mei 2016

Vanessa na shilole bado kizungu mkut

Zilianza kuandikwa siku ya May 17 2016 baada ya mastaa wawili kutoka kiwanda cha bongoflevani kurushiana maneno katika post zao walizozipost kwenye mtandao wa Instagram, Stori ilianzia kwenye Picha, lakini this time kila moja ameongea.Baada ya Shilole na Vanessa Mdee kurushiana Maneno kupitia Picha zao kila mmoja kwa time yake amezungumza na nakufunguka haya..Vanessa Mdee alifunguka maneno haya>>Nadhani nimeshasema kilakitu ambacho kinahitaji kusemwa kama umesoma post yangu utakuwaumeshaelewa kama hujasoma sawa sihitaji kurudia kitu’Shilole na yeye kuyafunguka haya>>’acha nimnyooshe kapanic kuona Say my name imetoka na mimi kuzinguliwa sitaki kuna mahalikaenda kuniongelea vibaya na asitamani kuonana na Shishi atatamani kuadithia vibao nilivyokuwa natoa somewhere

posted from Bloggeroid