Ijumaa, 13 Machi 2015

Faida ya juisi ya ukwaju

Ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu.

Ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili   linatumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana  kiafya.


Faida ya juisi ya ukwaju

Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya matumbo .

Huulinda mwili dhidi ya mafua 

Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula
 
Husaidia kutibu matatizo ya nyongo  

Husaidia kurahisisha choo (laxative)

Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na  kuimarisha moyo 

Husaidia ngozi kuwa nyororo,
 
Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

kwa wanaofanyiwa oparation ni nzuri sana inakausha kidonda kwa ndani kwa haraka . 


Jumatano, 11 Machi 2015

Watu 40 wamepoteza maisha kwajali ya gali mkoani iringa

Watu 41 wamefariki katika eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa,nyanda za juu kusini mwa Tanzania, baada ya basi la kampuni ya Majinja Express walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Lori.
Miili ya waliofariki katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Mafinga mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mvungi amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya hao 41 waliopoteza maisha,wanaume ni 33,wanawake watano na watoto watatu.
Akielezea chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Mvungi amesema kuwa dereva wa Lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara swala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana uso kwa uso.


Hata hivyo kasha la lori hilo liliangukia basi hilo la kampuni ya Majinja na kusababisha vifo kwa abiria hao.
Miili ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya Mafinga mkoani humo,na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Kwa mjibu wa kamanda mvungi taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusiana na ajali hiyo.
Kumekuwa na ajali za mara kwa mara za barabarani katika nchi za Afrika mashariki ambazo husababishwa na mwendo wa kasi wa madereva na ubovu wa barabara.


Jumapili, 8 Machi 2015

#MICHEZO Manchester United kumuuza Di Maria

Di Maria hajaonyesha umahiri wake tangu aliposajiliwa katika kilabu ya Manchester united kutoka Real Madrid na inaaminika kwamba yeye na mkewe hawajazoea maisha ya Manchester baada ya jaribio la wizi katika nyumba yao.
Wiki iliopita raia huyo wa Argentina ,mkewe Jorgelina Cardoso na mwanawe wa mwaka mmoja wamehamia katika nyumba ya aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Phil Nevile iliopo ghorofa ya 45.
Wamekodisha nyumba hiyo kwa kuwa Di Maria ana mpango m'badala wa maisha yake swala ambalo kilabu ya Manchester United inalifahamu.


Hatua hiyo inadaiwa kushinikiza harakati za kilabu hiyo kutaka kumsajili mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale.
Ijapokuwa Bale amekuwa akisema kuwa hataki kuondoka katika kilabu ya Real Madrid ili kurudi katika ligi ya Uingereza,United inahisi kwamba inaweza kum'bembeleza ili kubadilisha msimamo wake iwapo watakubaliana na mabingwa hao wa Ulaya.


Jumatano, 4 Machi 2015

Watu 42 kupoteza maisha na 82 kujeluhiwa kutokana na mvua kali na upepo mkali kusababisha mafuliko

Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82
kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali
kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata
wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi
imewaacha watu 3,500 bila makazi katika kaya
350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya
mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro
Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha
mafuruko katika kata ya Mwakata kuezua nyumba
na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya
ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na vyakula
kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika
hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi
ingawa wengine wanaendelea vizuri.


Jumapili, 1 Machi 2015

Mbunge jonh komba amefaliki dunia

Mbunge na Mwimbaji maaarufu wa nyimbo za Siasa nchini Tanzania, Keptain John Komba amefariki dunia siku ya jumamosi jioni.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama tawala cha Tanzania chama cha Mapinduzi Nape Nnauye Mbunge huyo ambaye alikuwa maarufu kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kampeni za chama hicho kifo cha chake kimetokea siku ya jumamosi majira ya jioni.
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.