Waziri wa wizara ya uchukuzi amemsimamisha
kazi kwa muda usiojulikana kaimu mkurugenzi
mkuu wa mamlaka ya bandari madeni kipande ili
kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali
zinazomkabili ikiwemo ukiukwaji wa taratibu za
manunuzi.
Tuhuma nyingine zinazomkabili ni mahusiano
yasoyoridhisha kati ya uongozi wa mamlaka hiyo
na wadau wake muhimu ambapo pia mara kadhaa
imetokea bodi inapopitisha mazabuni yeye
huchelewesha barua, huku tume ya watu sita
ikiundwa kuchunguza tuhuma hizo na Bw Awadhi
Massawe akiteuliwa kushika wadhifa huo.
Wakati huohuo kamati ya bunge ya hesabu za
serikali na mashirika ya umma PAC imeitaka
serikali kujenga bomba la kusafirisha mafuta
kwenda mikoani ili kuepusha uharibifu wa barabara
unaofanywa na malori yanayosafirisha mafuta ikiwa
ni pamoja na kuwa na matenki makubwa ya umma
ya kuhifadhia mafuta ili kupunguza msongamano
wa meli za mafuta baharini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Zitto Kabwe ametoa
wito huo mara baada ya kutembelea na kukagua
eneo linalotumika kupokelea mafuta ambapo pia
wameishauri serikali kufikiria chanzo maalum cha
mapato kwa ajili ya ujenzi wa reli akitolea mfano
nchi ya Kenya ambayo hutumia mapato ya kodi za
bidhaa zinazotoka nje kupanua reli yao.
Akijibu maswali mbalimbali ya wajumbe wa kamati
hiyo kaimu mkurugenzi wa TPA Bw Awadhi
Massawe amesema asilimia 90 ya mizigo yote
inayotoka bandarini inasafirishwa kwa njia ya
barabara hivyo ni vyema serikali ikaweka mkazo
kwenye ujenzi wa mabomba hayo pamoja na
uimarishwaji wa miundombinu ya reli huku
mwakilishi kutoka tra akielezea utaratibu
unaotumika kukusanya kodi.
Jumatatu, 16 Februari 2015
Waziri wa wizara ya uchukuzi amemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana kaimu mkurugezi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni