Ijumaa, 6 Februari 2015

CUF ya wahimiza wananchi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura na kuunga mkono maazimio ya UKAWA.


Chama cha wananchi CUF katika mikoa ya lindi na
mtwara, kimewataka wananchi wa mikoa hiyo
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la
kudumu la wapiga kura, ili waweze kushiriki
kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.
Rai hiyo imetolewa na viongozi wa chama hicho
katika mkutano wa hadhara mjini lindi, uliofanyika
kwa malengo ya kuwaelimisha wananchi juu ya
umuhimu wa kushiriki katika zoezi la kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Viongozi wa chama cha wananchi CUF kanda ya
kusini wakizungumza na wananchi katika eneo la
sabasaba mjini lindi wametumia fursa hiyo
kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga
kura ili kuweza kupata haki yao ya kikatiba ya
kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu mwaka
huu.
Aidha viongozi hao pia wametumia nafasi hiyo
kuwaomba wananchi kuunga mkono msimamo
uliotolewa na vyama vya upinzani vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi ukawa,wa kutoshiriki
katika zoezi la kupigia kura rasimu
inayopendekezwa mpaka hapo muda na elimu ya
kutosha vitakapotolewa kwa wananchi.
Hata hivyo #uhondo ikataka kujiridhisha iwapo wananchi
katika maeneo hayo wanauelewa wa kutosha
kuhusu elimu ya katiba, ambapo wamedai kuwa
licha ya kutoifahamu rasimu pendekezwa
inayozungumziwa sasa, hata hiyo ya zamani pia
hawajahi kuitia machoni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni