Kesi inayomkabili kiongozi wa jumuiya na taasisi
ya kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda
imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro huku jeshi la polisi
likilazimika kuwadhibiti wafuasi wa shekhe Ponda
nje ya uzio wa mahakama.
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ni aliyekuwa
mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro (OCD) Sadick
Tindwa ambaye kwa sasa ni OCD wilaya ya
Handeni mkoani Tanga ametoa ushahidi wake kwa
zaidi ya saa mbili ambapo ameieleza mahakama
kuwa julai 31 mwaka 2013 akiwa OCD wilaya ya
Morogoro alipokea barua kutoka kwa umoja wa
wahadhiri wa dini ya kiislamu wakiomba kufanya
kongamano la siku kuu ya Eid pili walilotaka
kufanya katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja
cha ndege manispaa ya Morogoro Agosti 9 mwaka
2013.ambapo alitoa kibali kwa masharti ya kufanya
kongamano hilo kwa kutokuao maneno ya kashfa
dhidi ya dini nyingine.
Aidha amesema katika kongamaono hilo wahadhiri
mbalimbali walitoa mada ambapo msemaji wa
mwisho alikuwa ni mshtakiwa Ponda Issa Ponda
na wakati akiendelea kuzungumza alitoa maneno
yenye mtazamo ya uchochezi, kashfa na kuumiza
imani za dini nyingine ambapo amesema serikali
ilipelekeka majeshi kwa wananchi wa Mtwara
wakati walikuwa wakidai haki yao kwenye gesi
lakini kwa kua asilimia kubwa ya wananchi wa
Mtwara ni wasilaaam lakini serikali ilishindwa
kupeleka majeshi kwenye mgogoro wa loliondo
kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa
lolindo ni wakaristu.
Uchochezi mwingine umedaiwa kuwa shekhe
Ponda aliwaambia waumini wa kiisalaam wasiunge
mkono kamati za ulinzi na usalama za dini kwani
zimeundwa na Bakwata pamoja na serikali kwa
manufaa yao binafsi, hivyo kamati hizo zikifika
katika misikiti na kujitambulisha wafunge milango
na madirisha kisha wawapige.
Upande wa utetezi wenye mawakili watatu
akiwemo wakili Juma Nasoro, Batheromeo Tarimo
na Abubakar Salimu wameuliza maswali ya msingi
ambayo , je nafasi gani aliyokuwa nayo sheikh
Ponda katika kongamano hilo, kuna uhusiano gani
kati ya mashtaka aliyofunguliwa sheikh Ponda na
maneno aliyotoa kwenye kongamano, kongamano
lilikuwa halali ama sio halali, mbali na jamhuri dini
je nigani iliwahi kulalamikia kuumizwa na maneno
aliyotoa sheikh Ponda siku ya kongamanona ? Na
kueleza kongamano lilikua halali na liliruhusiwa.
kesi hiyo imeahiriswa na itaendelea kusikilizwa
tena jan 27 mwaka huu katika mahakama ya
hakim mkazi mkoani Morogoro.
Jumanne, 27 Januari 2015
Kesi ya sheikh ponda kusikilizwa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni