Jumanne, 27 Januari 2015

Kesi ya sheikh ponda kusikilizwa


Kesi inayomkabili kiongozi wa jumuiya na taasisi
ya kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda
imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro huku jeshi la polisi
likilazimika kuwadhibiti wafuasi wa shekhe Ponda
nje ya uzio wa mahakama.
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ni aliyekuwa
mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro (OCD) Sadick
Tindwa ambaye kwa sasa ni OCD wilaya ya
Handeni mkoani Tanga ametoa ushahidi wake kwa
zaidi ya saa mbili ambapo ameieleza mahakama
kuwa julai 31 mwaka 2013 akiwa OCD wilaya ya
Morogoro alipokea barua kutoka kwa umoja wa
wahadhiri wa dini ya kiislamu wakiomba kufanya
kongamano la siku kuu ya Eid pili walilotaka
kufanya katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja
cha ndege manispaa ya Morogoro Agosti 9 mwaka
2013.ambapo alitoa kibali kwa masharti ya kufanya
kongamano hilo kwa kutokuao maneno ya kashfa
dhidi ya dini nyingine.
Aidha amesema katika kongamaono hilo wahadhiri
mbalimbali walitoa mada ambapo msemaji wa
mwisho alikuwa ni mshtakiwa Ponda Issa Ponda
na wakati akiendelea kuzungumza alitoa maneno
yenye mtazamo ya uchochezi, kashfa na kuumiza
imani za dini nyingine ambapo amesema serikali
ilipelekeka majeshi kwa wananchi wa Mtwara
wakati walikuwa wakidai haki yao kwenye gesi
lakini kwa kua asilimia kubwa ya wananchi wa
Mtwara ni wasilaaam lakini serikali ilishindwa
kupeleka majeshi kwenye mgogoro wa loliondo
kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa
lolindo ni wakaristu.
Uchochezi mwingine umedaiwa kuwa shekhe
Ponda aliwaambia waumini wa kiisalaam wasiunge
mkono kamati za ulinzi na usalama za dini kwani
zimeundwa na Bakwata pamoja na serikali kwa
manufaa yao binafsi, hivyo kamati hizo zikifika
katika misikiti na kujitambulisha wafunge milango
na madirisha kisha wawapige.
Upande wa utetezi wenye mawakili watatu
akiwemo wakili Juma Nasoro, Batheromeo Tarimo
na Abubakar Salimu wameuliza maswali ya msingi
ambayo , je nafasi gani aliyokuwa nayo sheikh
Ponda katika kongamano hilo, kuna uhusiano gani
kati ya mashtaka aliyofunguliwa sheikh Ponda na
maneno aliyotoa kwenye kongamano, kongamano
lilikuwa halali ama sio halali, mbali na jamhuri dini
je nigani iliwahi kulalamikia kuumizwa na maneno
aliyotoa sheikh Ponda siku ya kongamanona ? Na
kueleza kongamano lilikua halali na liliruhusiwa.
kesi hiyo imeahiriswa na itaendelea kusikilizwa
tena jan 27 mwaka huu katika mahakama ya
hakim mkazi mkoani Morogoro.

Jumatatu, 26 Januari 2015

Mh dk magufuri amesema kwamba hata kama serikali itajenga barabara nyingi kiasigani


Waziri wa ujenzi Mh Dk John Magufuli amesema
hata kama serikali itajenga barabara nyingi kiasi
gani lakini barabara hizo zikigeuza kuwa ni
sehemu ya kufanyia biashara tatizo la foleni katika
jiji la Dar es Saalam halitakwisha hivyo ameagiza
watu wote wanaoafanya hivyo hatua kali dhidi yao
zichuliwe.
Mh Magufukli ameyasema hapo katika zira yake ya
kukagua ujenzi wa barabra mbalimbali katika jini la
Dar es Salaam ambapo amesema inashangaza
kona kuwa mabilioni ya fedha yanatumika kujenga
barabara tena kwa kodi a wananchi huku baadhi
ya watu wanazihujumu hizo barabra.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Bw Said Meki Sadik ameziagiza
halmashauri zote za mkoa kuhakisha kuwa katika
bajeti ya mwaka huu wahakishe wanaongeza bajeti
ya ujenzi wa barabara na kama hawatafanya hivyo
hatozipitisha bajeti zao.
Partick Mfugale ni mtendaji mkuu wa wakala wa
barabara nchini amesema miradi mingi inakwenda
vizuri ila changamoto kubwa ni serikali kuchelewa
kutoa fedha tatizo ambalo linachelewesha ujenzi
wa barabara.
Akizungumza katika uzinduzi huo mbunge wa
ubungo Mh Johm Mnyika amepongeza hatua
iliyofikiwa na kusema kuwa kama barabra hizo
zitakamilika zitasaidia kupunguza msongamano
wa foleni huku mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es
Salaam Mh Ramadhnai Madabida akiahidi kuibana
serikali katika kutekeleza ahadi zake.

 uhondoleo.blogsport.com 

Jumapili, 25 Januari 2015

serekali imesema itawachukulia shelia kari wavuvi halam


Serikali imesema itawachukulia hatua za kisheria
wanaojihusisha na uvuvi haramu unaochangia
kuharibu mazalia ya viumbe vya bahari na
uharibifu wa mazingira.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mheshimiwa SANING'O OLE TELELE a mesema
mjini Mtwara uvuvi wa kutumia baruti unapaswa
kupigwa vita kwa nguvu zote na hatua za kisheria
zinapaswa kuchukuliwa kwa wanaofanya hivyo ili
kulinda mazingira ya bahari na viumbe vyake.
Mheshimiwa OLE TELELE ametoa onyo hilo baada
ya kupewa taarifa na wahifadhi wa bahari juu ya
vitendo vya uharibifu wa mazingira vinavyofanywa
na wavuvi.
Katika taarifa yake Mhifadhi Mkuu wa Bahari
Ghuba ya Mnazi Bay na Mto Ruvuma Bwana
REDFRED NGOW amesema uchumi wa wakazi wa
pwani ya Mtwara unategemea bahari,lakini watu
wachache wamekuwa wakivuruga chanzo hicho.

Jumamosi, 24 Januari 2015

RAIS ATANGAZA MAWAZILI WAPYA 8


Rais Jakaya kikwete  ametangaza
mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja
na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya
rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri
wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye
amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa
waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya
kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya
ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu
pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo
imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa
ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii
leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga
ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais]
mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa
afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na
makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na
ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa
rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na
makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya
kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini

MANCHESTEN UNITED YATOKA SARE NA KLABU YA LIGI DALAJA LA PILI


Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal
amesema kuwa kila kitu kilikwenda kinyume na
matarajio ya timu hiyo wakati wa sare ya 0-0 dhidi
ya timu ya Cambridge United katika kombe la FA
raundi ya nne.
Radamel Falcao na Angel Di Maria wote walikosa
mabao katika uga wa Abbey.
Lakini kikosi cha Van Gaal kilishindwa kuibwaga
miamba hiyo ya ligi ya daraja la pili na kulazimika
kukutana nao tena nyumbani Old Trafford.
''Kila kitu kilikwenda kinyume na matarajio yetu,si
uwanja refa ...yani kila kitu'',alisema Van Gaal.

Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu kufuatia sakata la Escrow.


Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter
Muhongo amejiuzulu kufuatia sakata la Escrow.

Professa Muhongo alitoa tanagazo hilo wakati wa
mkutano na vyombo vya habari.
Kujiuzulu kwake kunajiri baada ya kufutwa kazi
kwa waziri wa Ardhi na kujiuzulu kwa mwanasheria
mkuu ,wote wakiwa wamehusishwa na kutolewa
kwa zaidi ya dola milioni 120 kutoka kwa benki
kuu ya taifa hilo kupitia mazingira ya kutatanisha.

Ijumaa, 23 Januari 2015

UKAWA WAMEWATAKA WANANCHI WANAUNGA KATIBA


Viongozi wakuu wa vyama vinavyuounda umoja wa katiba ya wananchi -UKAWA- wamewataka wananchi wanaowaunga mkono umoja huo kutoshiriki katika zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa linalotarajiwa kufanya mapema mwezi aprili mwaka huu kutokana na mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba hiyo inayopendekezwa ulikuwa batili.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa mwenza wa umoja huo Prof  Ibrahimu Lipumba amesema UKAWA hawawezi kushiriki katika kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa ambayo haijapatikana katika misingi ya kidemokrasia pamoja na ukiukwaji wa makubaliano ambapo awali kupitia kituo cha demokrasia-TDC- walikubaliana na Mhe.Rais kwamba zoezi hilo lifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge jambo ambalo halikutekelezwa.
 
Kwa upande wake, mwenyekiti mwenza mweshimiwa Freeman Mbowe amesema mpaka sasa ziko katiba pendekezwa zaidi ya nne mitaani, jambo linalozidi kuwachanganya wananchi, na kusisitiza kuwa  haiwezekani daftari ya kudumu la wapiga kuwa tayari kabla ya mwezi aprili ambapo pia ameitupia lawama tume ya taifa ya uchaguzi-NEC- kwa kuwashirikisha wafadhili katika changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa kupiga kura kielektroniki badala ya kuwashirikisha wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa.
 
Aidha mwenyekiti mwenza Bwana James Mbati amedai kushtushwa na zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa kufanyia mapema mwezi aprili wakati wananchi hawajapata elimu ya kutosha, hakuna daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na viongozi wa vyama kutopatiwa katiba inayopendekezwa na kusistiza umoja huo sasa umejiekeza zaidi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu. 
 

Jumatatu, 19 Januari 2015

MUME AKIRI KUMCHINJA MKEWE LONDON


Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini London.
Naveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.
Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.


Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.

MAFULIKO YAWAUWA WATU 200


Utawala nchini Malawi unasema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo.
Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.
Takriban watu 200 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine 200,000 wakilazimika kuhama makwao.
Serikali ya msumbiji imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira chakula maji na makao.

WATU 14 WAKAMATWA KWAKUWACHOMA MOTO WANAUME 3


 Watu 14 wamekamatwa katika jimbo la Bihar Kaskazini mwa India baada ya kushukiwa kuwachoma moto watu watatu wakiwa hai pamoja na nyumba zao India na kusababidha ghasia Jumapili katika mtaa wa Ajitpur eneo la Muzaffarpur. Inaarifiwa zilichochewa na kupatikana kwa mwili wa mwanamume wa kihindu katika kijiji hicho zaidi ya wiki moja baada ya mwanamume huyo kutoweka. Afisaa mmoja wa polisi, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana muisilamu. Inaarfiwa alitekwa nyara na kuuawa. Umati mkubwa ulikusanyika katika eneo hilo baada ya mwili kupatikana na kuanza kuteketeza nyumba zaidi ya kumi huku watu watatu wakiuawa. Hali katika eneo hilo ni mbaya ingawa polisi wameweza kuidhibiti. Maafisa wanasema babake mwanamue huyo, aliwasilisha malalamiko kwa polisi huku akidai kuwa mwanawe alitekwa nyara. Jimbo la Bihara limeamrisha kufanywa uchunguzi huku mamia ya polisi wakishika doria katika eneo hilo. Idadi ya wahindu nchini India ni asilimia 80 ikilinganishwa na waisilamu ambao ni asilimia 14 ya watu bilioni 1.2 nchini humo. Wadadisi wanasema jamii hizo huishi kwa amani lakini kuna nyakati fulani ambapo wao huvurugana. Mnamo septemba mwaka jana takribna watu 50 walifariki katika vurugu kati ya wahindu na waisilamu katika eneo la Muzaffzarnagar. 

Jumapili, 18 Januari 2015

Wanafunzi 48 wasichana wa shule ya sekondari ya Muungano wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto,Kilimanjar


Wanafunzi 48 wasichana wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya vipaji maalum ya Muungano wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na vifaa vyao vyote.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ya wananchi Mh Zawadiel Maruchu amesema, moto huo ulianza kwenye bweni hilo kuanzia saa moja usiku wakati wanafunzi wakijiandaa kupata chakula lakini hamna aliyejeruhiwa.
 
Mh Maruchu amevipongeza vyombo vya ulinzi, zima moto na wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa uliofanikisha kuzimwa kwa moto huo ambao umetekeza vifaa vyote ingawa kuna mabaki kidogo ya nguo.
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Bw Flugence Mponji amesema, wanafunzi wa kidato hicho wamerudishwa nyumbani kwao kwa wiki moja wakati serikali inafanya juhudi za haraka kuwatafutia malazi.
 
Wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali iimarishe ulinzi na kuweka uzio wa shule na kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi miongoni mwa wananchi wa kata ya kilema kusini.
 
Wazazi wa wanafunzi hao wameiomba serikali iweke miundo mbinu yenye hadhi ya shule hiyo kuwa ya bweni ya wasichana wa vipaji maalum kuliko hali ilivyo sasa ambayo mazingira yake ni hatarishi.