Ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu.
Ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili linatumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana kiafya.
Faida ya juisi ya ukwaju
Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya matumbo .
Huulinda mwili dhidi ya mafua
Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula
Husaidia kutibu matatizo ya nyongo
Husaidia kurahisisha choo (laxative)
Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na kuimarisha moyo
Husaidia ngozi kuwa nyororo,
Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
kwa wanaofanyiwa oparation ni nzuri sana inakausha kidonda kwa ndani kwa haraka .
Ijumaa, 13 Machi 2015
Faida ya juisi ya ukwaju
Jumatano, 11 Machi 2015
Watu 40 wamepoteza maisha kwajali ya gali mkoani iringa
Watu 41 wamefariki katika eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa,nyanda za juu kusini mwa Tanzania, baada ya basi la kampuni ya Majinja Express walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na Lori.
Miili ya waliofariki katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Mafinga mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mvungi amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya hao 41 waliopoteza maisha,wanaume ni 33,wanawake watano na watoto watatu.
Akielezea chanzo cha ajali hiyo, Kamanda Mvungi amesema kuwa dereva wa Lori alijaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara swala lililomsababisha kutoka katika upande wake wa barabara hadi upande wa basi hilo na kusababisha kugongana uso kwa uso.
Hata hivyo kasha la lori hilo liliangukia basi hilo la kampuni ya Majinja na kusababisha vifo kwa abiria hao.
Miili ya waliofariki katika ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya Mafinga mkoani humo,na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Kwa mjibu wa kamanda mvungi taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusiana na ajali hiyo.
Kumekuwa na ajali za mara kwa mara za barabarani katika nchi za Afrika mashariki ambazo husababishwa na mwendo wa kasi wa madereva na ubovu wa barabara.
Jumapili, 8 Machi 2015
#MICHEZO Manchester United kumuuza Di Maria
Di Maria hajaonyesha umahiri wake tangu aliposajiliwa katika kilabu ya Manchester united kutoka Real Madrid na inaaminika kwamba yeye na mkewe hawajazoea maisha ya Manchester baada ya jaribio la wizi katika nyumba yao.
Wiki iliopita raia huyo wa Argentina ,mkewe Jorgelina Cardoso na mwanawe wa mwaka mmoja wamehamia katika nyumba ya aliyekuwa mchezaji wa Manchester United Phil Nevile iliopo ghorofa ya 45.
Wamekodisha nyumba hiyo kwa kuwa Di Maria ana mpango m'badala wa maisha yake swala ambalo kilabu ya Manchester United inalifahamu.
Hatua hiyo inadaiwa kushinikiza harakati za kilabu hiyo kutaka kumsajili mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale.
Ijapokuwa Bale amekuwa akisema kuwa hataki kuondoka katika kilabu ya Real Madrid ili kurudi katika ligi ya Uingereza,United inahisi kwamba inaweza kum'bembeleza ili kubadilisha msimamo wake iwapo watakubaliana na mabingwa hao wa Ulaya.
Jumatano, 4 Machi 2015
Watu 42 kupoteza maisha na 82 kujeluhiwa kutokana na mvua kali na upepo mkali kusababisha mafuliko
Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82
kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali
kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata
wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi
imewaacha watu 3,500 bila makazi katika kaya
350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya
mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro
Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha
mafuruko katika kata ya Mwakata kuezua nyumba
na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya
ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na vyakula
kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika
hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi
ingawa wengine wanaendelea vizuri.
Jumapili, 1 Machi 2015
Mbunge jonh komba amefaliki dunia
Mbunge na Mwimbaji maaarufu wa nyimbo za Siasa nchini Tanzania, Keptain John Komba amefariki dunia siku ya jumamosi jioni.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama tawala cha Tanzania chama cha Mapinduzi Nape Nnauye Mbunge huyo ambaye alikuwa maarufu kwa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kampeni za chama hicho kifo cha chake kimetokea siku ya jumamosi majira ya jioni.
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
Ijumaa, 20 Februari 2015
Breaking news
kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya
nchini.
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania
Moses Bushagama maarufu kwa jina la Mez B
ambaye alikuwa muimbaji katika kundi la Chamber
Squard,inaelezwa kuwa amefariki Dunia leo asubuhi
wakati amelazwa katika hospitali ya mwananchi
mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Akizungumza baada ya kupigiwa simu Dada wa Mez
B amethibitisha kifo cha kaka yake ambapo
amesema ni muda hivi amekuwa akisumbuliwa wa
homa pamoja na tatizo la kuishiwa Damu na hivyo
walimpeleka katika hospitali ya GENERAL ambapo
hadi jana hali yake haikuwa mbaya sana leo ndio
kafikwa na umauti.Endelea kufuatilia taarifa zetu
tutakujuza.
kwa tasnia ya muziki wa kizazi kipya
nchini.
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania
Moses Bushagama maarufu kwa jina la Mez B
ambaye alikuwa muimbaji katika kundi la Chamber
Squard,inaelezwa kuwa amefariki Dunia leo asubuhi
wakati amelazwa katika hospitali ya mwananchi
mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Akizungumza baada ya kupigiwa simu Dada wa Mez
B amethibitisha kifo cha kaka yake ambapo
amesema ni muda hivi amekuwa akisumbuliwa wa
homa pamoja na tatizo la kuishiwa Damu na hivyo
walimpeleka katika hospitali ya GENERAL ambapo
hadi jana hali yake haikuwa mbaya sana leo ndio
kafikwa na umauti.Endelea kufuatilia taarifa zetu
tutakujuza.
Jumatatu, 16 Februari 2015
Waziri wa wizara ya uchukuzi amemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana kaimu mkurugezi
Waziri wa wizara ya uchukuzi amemsimamisha
kazi kwa muda usiojulikana kaimu mkurugenzi
mkuu wa mamlaka ya bandari madeni kipande ili
kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali
zinazomkabili ikiwemo ukiukwaji wa taratibu za
manunuzi.
Tuhuma nyingine zinazomkabili ni mahusiano
yasoyoridhisha kati ya uongozi wa mamlaka hiyo
na wadau wake muhimu ambapo pia mara kadhaa
imetokea bodi inapopitisha mazabuni yeye
huchelewesha barua, huku tume ya watu sita
ikiundwa kuchunguza tuhuma hizo na Bw Awadhi
Massawe akiteuliwa kushika wadhifa huo.
Wakati huohuo kamati ya bunge ya hesabu za
serikali na mashirika ya umma PAC imeitaka
serikali kujenga bomba la kusafirisha mafuta
kwenda mikoani ili kuepusha uharibifu wa barabara
unaofanywa na malori yanayosafirisha mafuta ikiwa
ni pamoja na kuwa na matenki makubwa ya umma
ya kuhifadhia mafuta ili kupunguza msongamano
wa meli za mafuta baharini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Zitto Kabwe ametoa
wito huo mara baada ya kutembelea na kukagua
eneo linalotumika kupokelea mafuta ambapo pia
wameishauri serikali kufikiria chanzo maalum cha
mapato kwa ajili ya ujenzi wa reli akitolea mfano
nchi ya Kenya ambayo hutumia mapato ya kodi za
bidhaa zinazotoka nje kupanua reli yao.
Akijibu maswali mbalimbali ya wajumbe wa kamati
hiyo kaimu mkurugenzi wa TPA Bw Awadhi
Massawe amesema asilimia 90 ya mizigo yote
inayotoka bandarini inasafirishwa kwa njia ya
barabara hivyo ni vyema serikali ikaweka mkazo
kwenye ujenzi wa mabomba hayo pamoja na
uimarishwaji wa miundombinu ya reli huku
mwakilishi kutoka tra akielezea utaratibu
unaotumika kukusanya kodi.
Mkoani tanga hofu ikitanda kufwatia sakata la ugaidi
Jeshi la polisi mkoani Tanga limesema linafanya
uchunguzi wa kina kuhusu tukio la vikundi vya
uhalifu kuweka kambi katika mapango ya mleni maji
moto yaliyopo eneo la amboni jijini Tanga kufuatia
sehemu kubwa ya wananchi kulihusisha tukio hilo
na vitendo vya ugaidi hatua ambayo inawapa hofu
wananchi kuhusu usalama wao.
Jumamosi, 7 Februari 2015
Wanamgambo 27 wauawa misri
Wanamgambo 27 wa kiislamu wameuawa kwenye oparesheni kubwa iyoendeshwa na jeshi la Misri katika eneo la Sinai Kaskazini.
Taarifa zinasema kuwa ndege za helikopta zilitumiwa kuwalenga wapiganaji hao ambao wametangaza kulitii kundi la Islamic State.
Ripoti zinasema kuwa wanajeshi wa Misri baadaye waliwaua kwa kuwapiga risasi wanachama 20 wa kundi hilo.
Kundi hilo linasema kuwa liliwavizia wanajeshi wa Misri mwezi uliopita ambapo zaidi ya wanajeshi 30 waliuawa.
Posted via Blogaway
Kamati ya nidhamu ya TFF yatoa hukumu Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa adhabu kwa watu tisa wakiwemo viongozi, wachezaji na kocha mmoja kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kinidhamu.
Katika kikao chake kilichofanyika juzi (Februari 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Kamati hiyo imewafungia mwaka mmoja viongozi wawili wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza kwa kuwashawishi wachezaji wa Mwanza Queens kugomea uamuzi halali. Sophia Tigalyoma (Mwenyekiti) na Katibu wake Hawa Bajanguo walitiwa hatiani kwa kuwashawishi wachezaji kugomea uamuzi wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF kutupa rufani yao dhidi ya Kigoma. Kocha wa Polisi Tabora, Eliakim Christopher amefungiwa mechi kumi na kupigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa Kanuni ya 39(2) ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kutiwa hatiani kwa kumtukana refa wakati wa mechi kati ya timu yake na Panone FC iliyochezwa mjini Moshi. Wachezaji wa JKT Oljoro FC, Dihe Makonga, Swaleh Idd Hussein, Ramadhan Mnyambegu na nahodha Shaibu Nayopa wamefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 300,000 kila mmoja kwa kuzingatia kanuni ya 36(10) ya FDL kutokana na kufanya vurugu kwenye mechi kati yao na Burkina Faso iliyochezwa mjini Morogoro. Mtunza Vifaa (Kit Man) wa JKT Oljoro FC, Eliud Mjarifu amefungiwa miezi sita na kupigwa faini ya sh. 200,000 kwa kumpiga Kocha wa Burkina Faso, CR Mwakambaya kwenye mechi kati ya timu hizo iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Pia Mjarifu amepewa onyo kali na kutakiwa kutorudia tena kutenda kosa, kwani hata mwenendo wake wakati wa shauri hilo ulionyesha utovu wa nidhamu mbele ya Kamati. Naye Mtunza Vifaa wa Rhino Rangers FC, Albert Mbuji amefungiwa miezi sita na faini ya sh. 200,000 kwa kupatikana na hatia ya kuwatukana na kugomea uamuzi wa marefa kwenye mechi dhidi ya Polisi Dodoma. Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya FDL. Kamati hiyo imeondoa malalamiko dhidi ya Ofisa Habari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire kwa vile refa Israel Mujuni Nkongo ambaye ni mlalamikaji hakufika kwenye shauri hilo. Nkongo alimlalamikia Bwire akidai alitoa maneno yenye kuweza kuchochea chuki dhidi yake kwa waamuzi, kwani kupitia redio 100.5 Times FM, Bwire alidai refa huyo ndiye aliyeshinikiza kuondolewa kwa refa Mohamed Theofil kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Pia Kamati hiyo imemkuta bila hatia Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda ambaye TFF ilimlalamikia kuwa akiwa mtendaji mkuu wa chama hicho alishindwa kuhakikisha timu ya Singida inaingia uwanjani kucheza na Dodoma kwenye mechi ya Kombe la Taifa kwa Wanawake. Kamati ilikubaliana na utetezi wa Gunda kuwa, jukumu la timu hiyo lilikuwa mikononi mwa viongozi wa TWFA Singida, na tayari SIREFA kupitia Kamati yake ya Nidhamu ilishatoa adhabu kwa viongozi wa timu hiyo kutokana na kitendo hicho. Nayo malalamiko ya Polisi Tabora FC kutaka mechi yao dhidi ya Toto Africans FC irudiwe kwenye uwanja huru (neutral ground) kwa madai ya kuchezeshwa zaidi ya muda unaotakiwa, na kutokuwepo ulinzi wa kutosha kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekataliwa. Pia Kamati ya Nidhamu imeelekeza malalamiko ya timu za Mwadui FC na Polisi Mara FC dhidi ya Toto Africans kwa kumchezesha mchezaji Ladislaus Mbogo bila kuonyesha leseni yake yasikilizwe haraka na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa vile si ya kinidhamu. Wakati huo huo, Kamati ya Nidhamu inaendelea na kikao chake leo (Februari 5 mwaka huu) kusikiliza malalamiko mengine ya kinidhamu yaliyofikishwa mbele yake.
MBUNGE AUWAWA NCHIN KENYA
PICHA HAPO JUU NIGARI LA MBUNGE⇧
Mbunge mmoja ameuawa kwa kupigwa risisi kwenye mji mkuu wa kenya Nairobi.
Ripoti za polisi zinasema kuwa mbunge huyo wa Kabete, eneo lililo nje kidogo ya mji wa Nairobi aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Walinzi wake wawili,dereva pia nao wameuawa.
Polisi wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha walilifuata gari la mbunge huyo kutoka eneo la Westlands kabla ya kulimiminia rasasi ndani ya mji wa Nairobi.
Ijumaa, 6 Februari 2015
CUF ya wahimiza wananchi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura na kuunga mkono maazimio ya UKAWA.
Chama cha wananchi CUF katika mikoa ya lindi na
mtwara, kimewataka wananchi wa mikoa hiyo
kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la
kudumu la wapiga kura, ili waweze kushiriki
kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao.
Rai hiyo imetolewa na viongozi wa chama hicho
katika mkutano wa hadhara mjini lindi, uliofanyika
kwa malengo ya kuwaelimisha wananchi juu ya
umuhimu wa kushiriki katika zoezi la kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Viongozi wa chama cha wananchi CUF kanda ya
kusini wakizungumza na wananchi katika eneo la
sabasaba mjini lindi wametumia fursa hiyo
kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga
kura ili kuweza kupata haki yao ya kikatiba ya
kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu mwaka
huu.
Aidha viongozi hao pia wametumia nafasi hiyo
kuwaomba wananchi kuunga mkono msimamo
uliotolewa na vyama vya upinzani vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi ukawa,wa kutoshiriki
katika zoezi la kupigia kura rasimu
inayopendekezwa mpaka hapo muda na elimu ya
kutosha vitakapotolewa kwa wananchi.
Hata hivyo #uhondo ikataka kujiridhisha iwapo wananchi
katika maeneo hayo wanauelewa wa kutosha
kuhusu elimu ya katiba, ambapo wamedai kuwa
licha ya kutoifahamu rasimu pendekezwa
inayozungumziwa sasa, hata hiyo ya zamani pia
hawajahi kuitia machoni.
Jumanne, 27 Januari 2015
Kesi ya sheikh ponda kusikilizwa
Kesi inayomkabili kiongozi wa jumuiya na taasisi
ya kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda
imeanza kusikilizwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro huku jeshi la polisi
likilazimika kuwadhibiti wafuasi wa shekhe Ponda
nje ya uzio wa mahakama.
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ni aliyekuwa
mkuu wa polisi wilaya ya Morogoro (OCD) Sadick
Tindwa ambaye kwa sasa ni OCD wilaya ya
Handeni mkoani Tanga ametoa ushahidi wake kwa
zaidi ya saa mbili ambapo ameieleza mahakama
kuwa julai 31 mwaka 2013 akiwa OCD wilaya ya
Morogoro alipokea barua kutoka kwa umoja wa
wahadhiri wa dini ya kiislamu wakiomba kufanya
kongamano la siku kuu ya Eid pili walilotaka
kufanya katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja
cha ndege manispaa ya Morogoro Agosti 9 mwaka
2013.ambapo alitoa kibali kwa masharti ya kufanya
kongamano hilo kwa kutokuao maneno ya kashfa
dhidi ya dini nyingine.
Aidha amesema katika kongamaono hilo wahadhiri
mbalimbali walitoa mada ambapo msemaji wa
mwisho alikuwa ni mshtakiwa Ponda Issa Ponda
na wakati akiendelea kuzungumza alitoa maneno
yenye mtazamo ya uchochezi, kashfa na kuumiza
imani za dini nyingine ambapo amesema serikali
ilipelekeka majeshi kwa wananchi wa Mtwara
wakati walikuwa wakidai haki yao kwenye gesi
lakini kwa kua asilimia kubwa ya wananchi wa
Mtwara ni wasilaaam lakini serikali ilishindwa
kupeleka majeshi kwenye mgogoro wa loliondo
kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi wa
lolindo ni wakaristu.
Uchochezi mwingine umedaiwa kuwa shekhe
Ponda aliwaambia waumini wa kiisalaam wasiunge
mkono kamati za ulinzi na usalama za dini kwani
zimeundwa na Bakwata pamoja na serikali kwa
manufaa yao binafsi, hivyo kamati hizo zikifika
katika misikiti na kujitambulisha wafunge milango
na madirisha kisha wawapige.
Upande wa utetezi wenye mawakili watatu
akiwemo wakili Juma Nasoro, Batheromeo Tarimo
na Abubakar Salimu wameuliza maswali ya msingi
ambayo , je nafasi gani aliyokuwa nayo sheikh
Ponda katika kongamano hilo, kuna uhusiano gani
kati ya mashtaka aliyofunguliwa sheikh Ponda na
maneno aliyotoa kwenye kongamano, kongamano
lilikuwa halali ama sio halali, mbali na jamhuri dini
je nigani iliwahi kulalamikia kuumizwa na maneno
aliyotoa sheikh Ponda siku ya kongamanona ? Na
kueleza kongamano lilikua halali na liliruhusiwa.
kesi hiyo imeahiriswa na itaendelea kusikilizwa
tena jan 27 mwaka huu katika mahakama ya
hakim mkazi mkoani Morogoro.
Jumatatu, 26 Januari 2015
Mh dk magufuri amesema kwamba hata kama serikali itajenga barabara nyingi kiasigani
Waziri wa ujenzi Mh Dk John Magufuli amesema
hata kama serikali itajenga barabara nyingi kiasi
gani lakini barabara hizo zikigeuza kuwa ni
sehemu ya kufanyia biashara tatizo la foleni katika
jiji la Dar es Saalam halitakwisha hivyo ameagiza
watu wote wanaoafanya hivyo hatua kali dhidi yao
zichuliwe.
Mh Magufukli ameyasema hapo katika zira yake ya
kukagua ujenzi wa barabra mbalimbali katika jini la
Dar es Salaam ambapo amesema inashangaza
kona kuwa mabilioni ya fedha yanatumika kujenga
barabara tena kwa kodi a wananchi huku baadhi
ya watu wanazihujumu hizo barabra.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam Bw Said Meki Sadik ameziagiza
halmashauri zote za mkoa kuhakisha kuwa katika
bajeti ya mwaka huu wahakishe wanaongeza bajeti
ya ujenzi wa barabara na kama hawatafanya hivyo
hatozipitisha bajeti zao.
Partick Mfugale ni mtendaji mkuu wa wakala wa
barabara nchini amesema miradi mingi inakwenda
vizuri ila changamoto kubwa ni serikali kuchelewa
kutoa fedha tatizo ambalo linachelewesha ujenzi
wa barabara.
Akizungumza katika uzinduzi huo mbunge wa
ubungo Mh Johm Mnyika amepongeza hatua
iliyofikiwa na kusema kuwa kama barabra hizo
zitakamilika zitasaidia kupunguza msongamano
wa foleni huku mwenyekiti wa CCM mkoa Dar es
Salaam Mh Ramadhnai Madabida akiahidi kuibana
serikali katika kutekeleza ahadi zake.
uhondoleo.blogsport.com
Jumapili, 25 Januari 2015
serekali imesema itawachukulia shelia kari wavuvi halam
Serikali imesema itawachukulia hatua za kisheria
wanaojihusisha na uvuvi haramu unaochangia
kuharibu mazalia ya viumbe vya bahari na
uharibifu wa mazingira.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mheshimiwa SANING'O OLE TELELE a mesema
mjini Mtwara uvuvi wa kutumia baruti unapaswa
kupigwa vita kwa nguvu zote na hatua za kisheria
zinapaswa kuchukuliwa kwa wanaofanya hivyo ili
kulinda mazingira ya bahari na viumbe vyake.
Mheshimiwa OLE TELELE ametoa onyo hilo baada
ya kupewa taarifa na wahifadhi wa bahari juu ya
vitendo vya uharibifu wa mazingira vinavyofanywa
na wavuvi.
Katika taarifa yake Mhifadhi Mkuu wa Bahari
Ghuba ya Mnazi Bay na Mto Ruvuma Bwana
REDFRED NGOW amesema uchumi wa wakazi wa
pwani ya Mtwara unategemea bahari,lakini watu
wachache wamekuwa wakivuruga chanzo hicho.
Jumamosi, 24 Januari 2015
RAIS ATANGAZA MAWAZILI WAPYA 8
Rais Jakaya kikwete ametangaza
mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja
na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya
rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri
wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye
amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa
waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya
kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya
ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu
pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo
imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa
ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii
leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga
ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais]
mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa
afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na
makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na
ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa
rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na
makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya
kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini
MANCHESTEN UNITED YATOKA SARE NA KLABU YA LIGI DALAJA LA PILI
Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal
amesema kuwa kila kitu kilikwenda kinyume na
matarajio ya timu hiyo wakati wa sare ya 0-0 dhidi
ya timu ya Cambridge United katika kombe la FA
raundi ya nne.
Radamel Falcao na Angel Di Maria wote walikosa
mabao katika uga wa Abbey.
Lakini kikosi cha Van Gaal kilishindwa kuibwaga
miamba hiyo ya ligi ya daraja la pili na kulazimika
kukutana nao tena nyumbani Old Trafford.
''Kila kitu kilikwenda kinyume na matarajio yetu,si
uwanja refa ...yani kila kitu'',alisema Van Gaal.
Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu kufuatia sakata la Escrow.
Waziri wa nishati na madini profesa Sospeter
Muhongo amejiuzulu kufuatia sakata la Escrow.
Professa Muhongo alitoa tanagazo hilo wakati wa
mkutano na vyombo vya habari.
Kujiuzulu kwake kunajiri baada ya kufutwa kazi
kwa waziri wa Ardhi na kujiuzulu kwa mwanasheria
mkuu ,wote wakiwa wamehusishwa na kutolewa
kwa zaidi ya dola milioni 120 kutoka kwa benki
kuu ya taifa hilo kupitia mazingira ya kutatanisha.
Ijumaa, 23 Januari 2015
UKAWA WAMEWATAKA WANANCHI WANAUNGA KATIBA
Viongozi wakuu wa vyama vinavyuounda umoja wa katiba ya wananchi -UKAWA- wamewataka wananchi wanaowaunga mkono umoja huo kutoshiriki katika zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa linalotarajiwa kufanya mapema mwezi aprili mwaka huu kutokana na mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba hiyo inayopendekezwa ulikuwa batili.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa mwenza wa umoja huo Prof Ibrahimu Lipumba amesema UKAWA hawawezi kushiriki katika kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa ambayo haijapatikana katika misingi ya kidemokrasia pamoja na ukiukwaji wa makubaliano ambapo awali kupitia kituo cha demokrasia-TDC- walikubaliana na Mhe.Rais kwamba zoezi hilo lifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge jambo ambalo halikutekelezwa.
Kwa upande wake, mwenyekiti mwenza mweshimiwa Freeman Mbowe amesema mpaka sasa ziko katiba pendekezwa zaidi ya nne mitaani, jambo linalozidi kuwachanganya wananchi, na kusisitiza kuwa haiwezekani daftari ya kudumu la wapiga kuwa tayari kabla ya mwezi aprili ambapo pia ameitupia lawama tume ya taifa ya uchaguzi-NEC- kwa kuwashirikisha wafadhili katika changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa kupiga kura kielektroniki badala ya kuwashirikisha wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa.
Aidha mwenyekiti mwenza Bwana James Mbati amedai kushtushwa na zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa kufanyia mapema mwezi aprili wakati wananchi hawajapata elimu ya kutosha, hakuna daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na viongozi wa vyama kutopatiwa katiba inayopendekezwa na kusistiza umoja huo sasa umejiekeza zaidi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.
Jumatatu, 19 Januari 2015
MUME AKIRI KUMCHINJA MKEWE LONDON
Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe katika nyumba yao mjini London.
Naveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.
Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.
Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza kusikilizwa mwezi Oktoba.
MAFULIKO YAWAUWA WATU 200
Utawala nchini Malawi unasema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo.
Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.
Takriban watu 200 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine 200,000 wakilazimika kuhama makwao.
Serikali ya msumbiji imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira chakula maji na makao.
WATU 14 WAKAMATWA KWAKUWACHOMA MOTO WANAUME 3
Watu 14 wamekamatwa katika jimbo la Bihar Kaskazini mwa India baada ya kushukiwa kuwachoma moto watu watatu wakiwa hai pamoja na nyumba zao India na kusababidha ghasia Jumapili katika mtaa wa Ajitpur eneo la Muzaffarpur. Inaarifiwa zilichochewa na kupatikana kwa mwili wa mwanamume wa kihindu katika kijiji hicho zaidi ya wiki moja baada ya mwanamume huyo kutoweka. Afisaa mmoja wa polisi, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana muisilamu. Inaarfiwa alitekwa nyara na kuuawa. Umati mkubwa ulikusanyika katika eneo hilo baada ya mwili kupatikana na kuanza kuteketeza nyumba zaidi ya kumi huku watu watatu wakiuawa. Hali katika eneo hilo ni mbaya ingawa polisi wameweza kuidhibiti. Maafisa wanasema babake mwanamue huyo, aliwasilisha malalamiko kwa polisi huku akidai kuwa mwanawe alitekwa nyara. Jimbo la Bihara limeamrisha kufanywa uchunguzi huku mamia ya polisi wakishika doria katika eneo hilo. Idadi ya wahindu nchini India ni asilimia 80 ikilinganishwa na waisilamu ambao ni asilimia 14 ya watu bilioni 1.2 nchini humo. Wadadisi wanasema jamii hizo huishi kwa amani lakini kuna nyakati fulani ambapo wao huvurugana. Mnamo septemba mwaka jana takribna watu 50 walifariki katika vurugu kati ya wahindu na waisilamu katika eneo la Muzaffzarnagar.
Jumapili, 18 Januari 2015
Wanafunzi 48 wasichana wa shule ya sekondari ya Muungano wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto,Kilimanjar
Wanafunzi 48 wasichana wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya vipaji maalum ya Muungano wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na vifaa vyao vyote.
Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo ya wananchi Mh Zawadiel Maruchu amesema, moto huo ulianza kwenye bweni hilo kuanzia saa moja usiku wakati wanafunzi wakijiandaa kupata chakula lakini hamna aliyejeruhiwa.
Mh Maruchu amevipongeza vyombo vya ulinzi, zima moto na wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa uliofanikisha kuzimwa kwa moto huo ambao umetekeza vifaa vyote ingawa kuna mabaki kidogo ya nguo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Moshi Bw Flugence Mponji amesema, wanafunzi wa kidato hicho wamerudishwa nyumbani kwao kwa wiki moja wakati serikali inafanya juhudi za haraka kuwatafutia malazi.
Wanafunzi wa shule hiyo wameiomba serikali iimarishe ulinzi na kuweka uzio wa shule na kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi miongoni mwa wananchi wa kata ya kilema kusini.
Wazazi wa wanafunzi hao wameiomba serikali iweke miundo mbinu yenye hadhi ya shule hiyo kuwa ya bweni ya wasichana wa vipaji maalum kuliko hali ilivyo sasa ambayo mazingira yake ni hatarishi.